i-Base

Pregnancy – Swahili translation

This page is part of Pocket ART, an easy guide to HIV treatment.

Virusi Vya Ukimwi (VVU) na ujauzito

(A new Swahili translation of this leaflet about HIV and pregnancy).

Translation by Angelina Namiba and Dr. Melckzedeck K. Osore.


The text for this leaflet is also pasted below.

Virusi Vya Ukimwi (VVU) na ujauzito

(Januari 2018)

Kipeperushi hiki kinaeleza kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na afya ya wanawake.

Maelezo haya yanawahusu watu/mama wanaoishi Uingereza.

Maelezo zaidi (kwa lugha ya Kiingereza) yanapatikana hapa: i-base.info/guides/pregnancy


Kipeperushi kinajumuisha maelezo kuhusu:

  • Utungaji mimba (mshiriki mmoja akiwa hana VVU).
  • Afya ya mama.
  • Kutumia matibabu ya ART thidi ya ukimwi wakati wa ujauzito (ART – kwa lugha ya kiingereza ni Anti Retroviral Therapy – ambayo ni aina ya madawa yanayodhibiti ukuaji wa virusi).
  • Afya ya motto wako.

Je, watu walioambukizwa VVU wanaweza kupata au kuzaa watoto ambao hawana virusi?

Ndio.

  • Hii ni mojawapo ya faida nyingi za matibabu
    ya VVU (ART).
  • Unaweza kupata watoto ukiwa umeadhirika na VVU.
  • Tafadhali zungumza na daktari wako ikiwa umeamua kuwa mjamzito.
  • Katika nchi ya Uingereza, watu wanaoishi na VVU wanapaswa kupokea huduma na msaada sawa na watu wasio na VVU.
  • Hii ni pamoja na huduma ya kukusaidia kuwa mjamzito
  • ART inamlinda mshiriki wakati wa utungaji
    wa mimba ikiwa mwenziwe ana VVU
  • ART inamlinda mtoto dhidi ya VVU wakati wa ujauzito na wakati wa kuzaliwa

Kupanga ujauzito wako

Kupanga kupata ujauzito hakuna tofauti ikiwa wewe ni mwaathirika wa VVU au la.

Lakini ikiwa hivi karibuni imethibitishwa kua umeambukizwa VVU wakati wa ujauzito, kuna uwezekano unastahili msaada zaidi.

Ikiwa tayari una VVU, daktari anaweza kukuhudumia afya yako kabla hujapata ujauzito – na pia kukuchunguza kwa makini na kuufuatilia ujauzito wako.

Chagua wanahuduma wa afya pamoja na zahanati ya ujauzito ambayo inakupa usaidizi na inayouheshimu uamuzi wako wa kutaka kupata mtoto.

Kwa watu wengi, kupata ujauzito kwa kutumia njia ya kawaida ndio chaguo la kwanza.

(Idadi ya chembechembe za VVU katika damu ya muadhirika inajulikana kwa lugha ya Kiingereza kama “HIV Viral Load”). Ikiwa imethibitishwa ya kwamba muathirika wa VVU ana idadi finyu ya chembechembe za VVU mwilini, basi utumizi wa ART utazuia kuambukiza mtu ambaye hana VVU.

Hii idadi ndogo ya chembechembe za VVU inapaswa kwanza kuthibitishwa kwa miezi kadhaa kabla ya kuamua kusitisha matumizi ya kondomu (condom).

Kuamua kupata ujauzito kwa kutumia ile njia ya kawaida ni jambo ambalo washirika wote wawili wanastahili kulijadili na kukubaliana.

Daktari wako anaweza kukuelimisha uelewe lini unapoweza kupata mimba kulingana hasa na mzunguko wako wa hedhi.


“Nilipotambua/nilipoambiwa ya kwamba nina VVU sikubadilisha hisia yangu kuhusu uzazi maana siku zote nilitamani kuwa mzazi na niitwe mama.

Nilipoamua kupata mototo nilipokea msaada wa maadili na maelezo kutoka kwa kina mama wenzangu wanaoishi na VVU.

Hatimaye nilipopata hakikisho kuhusu mtoto wangu mrembo, wasiwasi wote ukanitoka, pamoja na hofu na kutokuwa na uhakika. Nikatambua thamani ya msemo wa subira yavuta heri!.”

– Angelina


Je, ART ni salama kwa mama?

Ndio.

  • Usajili wa maelfu ya mimba unathibitisha ya kwamba hakuna madhara yoyote makubwa kwa mtoto kutoka na matumizi ya ART.

Je, ART ni salama kwa mtoto?

Ndio.

  • Usajili wa maelfu ya mimba unathibitisha ya kwamba hakuna madhara yoyote makubwa kwa mtoto kutoka na matumizi ya ART.

Nitajifungua kwa njia ipi?

IIkiwa kiwango cha VVU mwilini mwa mama hakionekani baada ya matumizi ya ART ndani ya wiki 36, miongozo ya Uingereza inapendekeza kujifungua kwa kutumia njia ya kawaida ya uke.

Katika hali nyingine upasuaji uliyopangwa unapendekezwa, hasa wakati wa dharura.


Kulinda na kuhakikisha afya ya mama

Afya yako mwenyewe na matibabu yako
ni mambo muhimu
zaidi ya kuzingatia ili kuhakikisha unajifungua salama na kuzaa? mtoto mwenye afya

Hili ndilo jambo la muhimu kwanza, daima.


Kuzingatia na kufuatilia kumeza madawa ya ART kama ulivyoshauriwa na daktari wako ni muhimu sana.

Kuchelewachelewa kumeza dawa kunapunguza ufanisi wa dawa hadi kiwango ambacho makali yanapungua.

Kamwe usizidishe kipimo cha dawa maradufu ikiwa umesahau kutumia kipimo kimoja au dozi moja.


Kumlisha mtoto wako

VVU vinaweza kutoka kwa mama hadi mtoto kupitia maziwa ya kunyonyesha.

Katika nchi ya Uingereza matumizi ya chupa na maziwa ya kununua (formula milk) kumnyonyesha motto mchanga ni hakikisho kwamba motto wake hapati madhara.

Muhimu. Maelezo haya kuhusu jinsi ya kumlisha mtoto mchanga yanawahusu watu/mama wanaoishi Uingereza.

Katika inchi nyingine kwa mfano Afrika, ushauri ni tofauti, na akina mama wanashauriwa kunyonyesha.

Hii ni kwa sababu maji ambayo ni masafi na yaliyo salama yanahitajika kutayarisha maziwa ya chupa.

Iwapo maji sio salama, basi ni afadhali kunyonyesha. Lakini pale tu idadi ya chembechembe za VVU kwenye damu ya mama ni chache mno kutoweza kuonekana kwa utumizi  wa ART.

(Important. This information/guidance regarding infant feeding is intended for/is for people/mothers living in the UK.)


Orodhesha mambo unayotaka kujadiliana na daktari au maswali unayotaka kumuuliza ili ufaidike kikamilifu na ushauri wake kwa muda unaokufaa.


Kupokea kijitabu hiki cha kurasa 56 (katika lugha ya Kiingereza) tafadhali piga simu 020 7407 8488 au agiza kwa kutumia mtandao.

i-base.info/order

Tunajibu maswali kwa njia kwa kutumia barua pepe au mtandao.

i i-base.info/qa Tafadhali tupe maoni yako.

surveymonkey.com/r/5MHM2LN